Uhuru, anayejulikana na wafuasi wake kama "Njamba" neno la Kikikuyu, linalomaanisha, Shujaa, ni mgombea wa urais wa muungano wa Jubilee, ambao ni muungano wa vyama vya TNA chake Kenyatta, (URP) na (Narc). Mgombea mwenza wake ni William Ruto wakisaidiana na Charity Ngilu,
Mwalimu wake wa siasa ambaye ni Rais mstaafu, Daniel Moi alimuingiza katika siasa kwa mara ya kwanza na kumpendekeza kuwa mgombea wa urais licha ya kutokuwa na uzoefu wa kisiasa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2002.
Hata hivyo, Uhuru alishindwa pakubwa na mpinzani wake, Rais mwai Kibaki na hivyo kumfanya kuwa kiongozi rasmi wa upinzani bungeni.
Uhuru aliungana na Raila kupinga rasimu ya katiba iliyopendekezwa na Kibaki mwaka 2005, lakini baadaye wakatengana huku Uhuru akimuunga mkono Kibaki katika kugombea muhula wa pili.
Kibaki, alitangazwa mshindi katika uchaguzi uliokumbwa na utata mkubwa na punde baadaye akamteua uhuru kama waziri wa serikali za mitaa.
Baada ya kibaki na odinga kutia saini makubaliano kusitisha mapigano, Uhuru aliteuliwa kama mmoja wa manaibu wawili wa waziri mkuu na kisha baadaye akateuliwa kuwa waziri wa fedha. Lakini alijiuzulu baadaye baada ya kupatikana na makosa ya kujibu katika kesi yake ICC ya uhalifu wa kivita kuhusu ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007.
ICC, inamtuhumu kwa kupanga mashambulizi yaliyofanywa na kundi haramu ya Mungiki, Kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya kabila la wjaluo baada ya wale wa kabila lake wakikuyu kushambuliwa katika mkoa wa Rift Valley.
Ruto na Uhuru walijitetea vikali dhidi ya tuhuma za ICC, na kusema kuwa waziri mkuu Rail Odinga anapaswa kuwajibikIa ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mwaka 2007/2008
Kama Waziri wa Fedha, Kenyatta alikuwa katika Msitari wa mbele kuleta mageuzi katika wizara ya fedha na ambavyo serikali hufanya biashara zake. Hasa katika kupanga makadirio ya matumizi ya pesa za serikali kupitia mitandao ya kijamii.
Alikuwa waziri wa kwanza wa Kenya kuzindua ruwaza iliyoundwa kwa kuhusisha wananchi na kutilia mkazo katika kutumia mitandao ya kijamii katika uundaji wa sera za chama chake.
Kenyatta anaahidi kuleta mageuzi ya kijamii,kisiasa na kiuchumi na anawaalika wakenya wote kuhusika na uundaji wa sera za chama chake.
Pia anaahidi kutoa hekari milioni moja ya mashamba kwa ajili ya ukulima wa unyunyiziaji maji mimea na kupanua kilimo katika kipindi cha miaka mitano.
No comments:
Post a Comment