Aliyekuwa mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Kenya, Samuel Kivuitu amefariki.
Kivuti ndiye aliyesimamia uchaguzi wa Kenya mwaka 2007 ambao ulikumbwa na ghasia.Msemaji wa familia ya Kivuitu,aliyekuwa na umri wa miaka 74, alifariki Jumatatu baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.
Kifo chake kilitokea wiki moja kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika ukiwa utakuwa wa kwanza baada ya ule wa mwaka 2007 kusababisha vurugu ambapo zaidi ya watu elfu sita waliuawa na wengine kuachwa bila makao.
Ripoti iliyotolewa na serikali ya Kenya mwaka 2008 ilisema kuwa tume ya uchaguzi iliyosimamia uchaguzi mwaka 2007, haikuwa huru na yenye uwezo wa kuendesha uchaguzi huo.
Ripoti hiyo ilisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa na kasoro na kwamba ilikuwa vigumu kubaini mshindi wa uchaguzi wenyewe
Viongozi wa Kenya wanatumai kuwa katiba mpya pamoja na idara ya mahama iliyo huru na idara ya polisi itasaidia kuendesha uchaguzi huru.
No comments:
Post a Comment