Kofi Annan ametoa wito kwa Wakenya kuhakikisha kuwa nchi yao haikumbwi na ghasia wakati wa uchaguzi utaofanywa tarehe March.
Kofi Annan aliongoza shughuli za
kupatanisha baada ya ghasia zilizofuatia uchaguzi miaka mitano iliyopita
ambapo watu zaidi ya elfu-moja walikufa.
Amesema matukio ya ghasia ya karibuni na mvutano unaozidi kabla ya uchaguzi yanatia wasi-wasi mkubwa.
Siku kumi kabla ya uchaguzi Bwana Annan ametoa wito kwa viongozi wa siasa, dini na jamii walaani hatua au matamshi yanayokusudia kuwatenga watu na kuwachochea.
Ametaka mizozo yoyote baada ya uchaguzi ipelekwa mahakamani.
Juma hili hakimu mkuu wa Kenya, Willy Mutunga, alisema mahakimu wanakabili vitisho na bughudha.
Bwana Mutunga alisema majaji watano wameshambuliwa hivi kabla ya uchaguzi.
Hakimu Mutunga amesifiwa kwa jumla kwa kujaribu kusafisha mahakama ambayo yamehusishwa na rushwa.
Aliwalaumu wanasiasa kwamba wanahusika na vitisho hivyo na alisema majaji hawatakubali kutishwa na kundi la wale wanaotaka kuirejesha nchi nyuma.
No comments:
Post a Comment