Maonyesho ya filamu mia kadha
kutoka sehemu mbali-mbali za Afrika na Wafrika walioko ng'ambo,
zitaoneshwa katika tamasha kubwa ya utamaduni wa Afrika ambayo inaanza
Burkina Faso Jumamosi.
Tuzo kubwa kabisa - Stallion of Yennenga - hupewa filamu ambayo inaonesha maisha halisi kabisa ya Afrika.
Filamu 20 za habari hasa kutoka Morocco, Algeria, Angola na Senegal zinagombea tuzo hiyo.
Ingawa Misri haikujiandikisha kwenye mashindano hata hivyo itaonesha filamu ya msanii wa Misri, Khaled Sayed, iitwayo "Stories from Tahrir".
Inaangalia changamoto ambazo Wamisri wanakabili wanapogombania uhuru.
No comments:
Post a Comment