Abdel Fatah al Sisi ameapishwa
rasmi kama rais mpya wa Misri katika sherehe iliofanyika katika mahakama
ya kikatiba katika mji mkuu wa Cairo.
Baada ya wimbo wa taifa na kusomwa kwa Quran
,rais El sisi alikula kiapo chake ambapo aliahidi kuheshimu sheria na
maslahi ya raia wa misri.Alishinda uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita kwa wingi wa kura ijapokuwa idadi ya waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo ilikuwa chini ya asilimia 50.
Uchaguzi huo unajiri miezi michache tu baada ya kiongozi huyo kumpindua madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.
Mkuu huyo wa jeshi wa zamani ameanzisha msako dhidi ya wanaompinga mbali na kukipiga marufuku chama cha Morsi cha Muslim Brotherhood.
No comments:
Post a Comment