Wafanyikazi wa usafiri wa mjini
Sao Paulo wamepiga kura kuidhinisha mgomo wao uendelee kwa mda
usiojulikana licha ya uamuzi wa mahakama ya leba nchini humo, iliyokuwa
imewaamuru wafanyikazi hao kurudi kazini mara moja.
Koti ilikuwa imesema wakuu katika vyama vya
wafanyikazi hao wa usafiri wa mjini Metro, walikuwa wametumia mamlaka
yao vibaya kwa kuanzisha mgomo tangu alhamisi iliyopita.Huku nusu ya vituo vya usafiri vikiwa tayari vimefungwa, msongamano wa magari umezidi kuizonga Sao Paulo.
Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 12 ilhali serkali imesema itamudu nyongeza ya takrban asilimia 9.
No comments:
Post a Comment