Serikali ya Kenya imesema kwa sasa inawashikilia zaidi ya watu elfu nne kufuatia operesheni usalama nchini humo.
Msako huo wa kamatakamata ulianza baada ya
mashambulio ya magruneti wiki iliyopita katika eneo la Eastleigh jijini
Nairobi, ambalo wakaazi wake wengi ni wa jamii ya Kisomali.Wengi wa watuhumiwa ni Wasomali.
Wengi wao wanashikiliwa kwa siku tatu katika uwanja wa mpira wa Kasarani jijini Nairobi. Umoja wa Mataifa, makundi ya kutetea haki na ndugu wa watu waliokamatwa wamesema wamenyimwa nafasi ya kukutana na watuhumiwa hao.
Waziri wa mambo ya Ndani wa Kenya, Joseph Ole Lenku, amesema wale ambao hawana vitambulisho kuhusu ukaazi au uraia wao wa Kenya, watafikishwa mahakamani na huenda wakarejeshwa Somalia.
TEMBELEA,http://themonthlyjob.com/?refcod=10947
Utapata ajira ya chapuchapu
No comments:
Post a Comment