Urusi imeionya Ukraine kuancha
maandalizi yoyote ya kijeshi kusini na mashariki mwa nchi hiyo, ikisema
kwa kufanya hivyo kutaanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi
imesema Ukraine ilikuwa ikipanga kupeleka majeshi yake katika maeneo
hayo, ikituhumu kwamba makandarasi binafsi wa kijeshi wa Marekani ni
miongoni mwa watu waliokuwa katika mpango huo.Onyo la Urusi limekuja baada ya serikali ya Ukraine kusema kwamba wanaendesha operesheni dhidi ya ugaidi wakati wa usiku katika jengo la utawala katika mji wa mashariki ya Ukraine wa Kharkiv na kuwakamata watu sabini wanaoiunga mkono Urusi ambao waliliteka jengo hilo. Jumatatu, wanaharakati wanaopendelea kujiunga na Urusi kutoka majimbo ya Kharkiv na Donetsk wametangaza kujitenga na Ukraine. (Urusi imekanusha kuchochea kukosekana kwa utulivu na mawazo ya kujitenga kwa maeneo nchini Ukraine.)TEMBELEA.
http:/themonthyjob.com/?refcod=10947
No comments:
Post a Comment