Kwa ufupi
Ni matukio ambayo yameacha maswali mengi
zaidi ya majibu, huku wengine katika jamii wakisaka mchawi. Polisi na
hata vyama vya kijamii, kila mmoja akiibuka na msimamo wake. Hata hivyo,
si rahisi kusema ni lini jibu litapatikana!
Padri auawa Zanzibar kwa risasi
Tukio lingine ambalo lilishtua wengi ni la kuawa kwa Padri Evarist Mushi, Paroko wa Parokia ya Minara Miwili , Zanzibar. Yeye, aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani na kufa papo hapo na watu wasiojulikana asubuhi akielekea kanisani.

Msemaji wa Polisi Zanzibar, Inspekta Mohamed Mhina
alithibitisha tukio hilo huku akisisitiza kuwa uchunguzi wa kina zaidi
ungefanyika kuhakikisha waliofanya hilo wanachukuliwa hatua.
Mwingine apigwa risasi
Awali, Kabla ya kuuawa padri Mushi, padri mwingine, Ambrose Mkenda naye alipigwa risasi na watu wasiofahamika kwenye lango la nyumba yake maeneo ya Kitomondo mjini Zanzibar, ambako ndiko makazi yake yalipo akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha pekee yake.

Hali yake siyo nzuri kwani risasi aliyopigwa
imemdhuru maeneo ya mdomoni na hadi sasa bado hajaweza kuwa imara.
Waliompiga risasi padri huyo inasemekana ni watu waliokuwa kwenye
pikipiki, ambao walimvamia akisubiria afunguliwe geti kuingia nyumbani
kwake.
Katibu wa Mufti amwagiwa tindikali
Pia Zanzibar ilikumbwa na tukio la linalofanana na matukio hayo kwani kiongozi mwingine wa dini aliingia kwenye msukosuko.
Pia Zanzibar ilikumbwa na tukio la linalofanana na matukio hayo kwani kiongozi mwingine wa dini aliingia kwenye msukosuko.
Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil
Suleiman Soraga, alimwagiwa tindikali na watu wasiyojulikana huko
Magogoni Msumbiji Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Yussuf
Ilembo, alisema Sheikh Soraga alimwagiwa tindikali majira ya alfajiri
alipokuwa akifanya mazoezi ya viungo.
Ni kwamba wakati akifanya mazoezi, alimuona mtu
akifanya mazoezi akielekea mbele yake na baada ya kukutana uso kwa uso
alimmwagia tindikali na kumjeruhi sehemu za usoni na kifua kabla ya mtu
huyo kutoweka.
Dk Stephen Ulimboka
Kiongozi wa jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Stephen Ulimboka, saa sita usiku alitekwa, kupigwa na watu watatu wenye silaha na kisha kutupwa maeneo ya mabwepande ambapo aliokotwa na kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) jijini Dar es Salaam.

Wengi wanahoji sababu ya kutekwa Dk Ulimboka, hasa
kutokana na ukweli kwamba si mfanyabiashara…Nani alimteka kwa lipi? Ni
swali lisilo na jibu.
Dk Ulimboka aliwahi kuwaambia waandishi wa habari
na baadaye akasisitiza kauli hiyo kupitia wanasheria wake, Oktoba 2012,
kuwa aliyehusika na mipango ya kutekwa na kuteswa kwake ni Ofisa wa
Ikulu. Kama ni kweli, je, ofisa huyo alitumwa au alijituma ? Na je,
aliwahi kuhojiwa polisi ili Ikulu ijisafishe kutoka katika madai haya ya
Dk Ulimboka?
Waandishi wa habari wauawa
Baadhi ya waandishi wa habari waliouawa katika mazingira ya utata ni pamoja na wa Kituo cha Redio Kwizera wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Issa Ngumba (45) ambaye aliuawa kwa kunyongwa na kisha kupigwa risasi mkono wa kushoto.

No comments:
Post a Comment