Kwa ufupi
“Enzi za Nyerere kulikuwa na Usalama wa Taifa wa
kweli. Ulikuwa ukiwaza tu kufanya jambo fulani tayari umedakwa, sasa
hivi makundi ya kimafya yanajiimarisha nchini, ni jambo la hatari sana,”
Moshi. Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), kimependekeza kusukwa upya kwa Idara ya Usalama wa
Taifa kwa madai kuwa, imezidiwa mbinu na makundi ya kimafya.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Chadema wa
Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema alipokuwa akizungumza na gazeti hili
kutokana na matukio ya kutisha ya kutekwa na kuteswa kwa watu mbalimbali
nchini.
Lema alisema Idara ya Usalama wa Taifa ya wakati
wa utawala wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, ilifanya kazi yake
kwa ufanisi mkubwa kuliko ilivyo sasa.
alisema.
Lema alisema matukio ya kutekwa nyara na kuteswa
kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari, Dk Steven Ulimboka na wa Jukwaa
la Wahariri, Absolom Kibanda yasingeweza kutokea enzi za Mwalimu
Nyerere.
“Kwanza nalaani sana tukio hili la Kibanda na mimi
nasema vyombo vyetu vya usalama visipoimarisha vitengo vya Intelijensia
vitajikuta vikishindwa kuzuia makosa,” alisema Lema.
Alisema Usalama wa Taifa unapaswa kufanya kazi
kama CIA ya Martekani inayobaini mipango ya uhalifu kabla
haijatendeka.“Leo hii wahamiaji haramu wanaingia nchini kila siku kana
kwamba hatuna Intelijensia… watu wanatekwa na kuteswa…viongozi wa dini
wanauawa? Usalama wa Taifa uko wapi,” alihoji Lema.
Lema alisema enzi za Nyerere ilikuwa vigumu kumfahamu nani ni Usalama wa Taifa hali iliyowasaidia kujichanganya.
No comments:
Post a Comment