Kwa ufupi
- Maofisa watatu watimuliwa kwa tuhuma za ‘kupoteza’ dawa za kulevya,
- Ofisa mmoja kwa kuwapiga na kuwabambikizia kesi zisizo na dhamana wananchi,
- Kamishna msaidizi Mwandamizi kwa kudai na kujipatia fedha ili kuajiri.
- Ofisa mmoja kwa kuwapiga na kuwabambikizia kesi zisizo na dhamana wananchi,
- Kamishna msaidizi Mwandamizi kwa kudai na kujipatia fedha ili kuajiri.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi amewafukuza kazi maofisa watano wa Polisi na kumsimamisha kazi
kwa mwezi mmoja Kamishna msaidizi Mwandamizi wa jeshi hilo kutokana na
makosa mbalimbali.
Pia, Dk Nchimbi amewafukuza makuruta 95 waliokuwa
Chuo Cha Polisi (CCP), Moshi kutokana na kugundulika kutumia rushwa
kupata ajira.
Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi
aliyesimamishwa kwa mwezi mmoja ni Renatus Chalamila akihusishwa na
rushwa katika kuajiri.
Alisema taarifa za uchunguzi za kamishna huyo,
ambaye anashughulikia masuala ya ajira zimewasilishwa kwa Rais Jakaya
Kikwete, ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kumfukuza kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Nchimbi alisema maofisa watatu kati ya hao watano wamefukuzwa kutokana na kugundulika kuwa walikamata dawa za kulevya aina ya cocaine lakini zilipopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali alidai zilikuwa ni chumvi na sukari.

“Kama mtakumbuka mkoani Mbeya, Aprili mwaka jana
zilikamatwa kilo 1.9 za dawa za kulevya na polisi walithibitisha hilo
lakini zilipopelekwa kwa Mkemia Mkuu zikagundulika ni chumvi na sukari,”
alisema na kuongeza:
“Niliunda timu kuchunguza kama ni kweli kwa kuwa askari walituthibitishia ni dawa za kulevya, timu ilichunguza na kugundua kilichokamatwa hakikuwa kilichopelekwa kwa Mkemia Mkuu.”
“Niliunda timu kuchunguza kama ni kweli kwa kuwa askari walituthibitishia ni dawa za kulevya, timu ilichunguza na kugundua kilichokamatwa hakikuwa kilichopelekwa kwa Mkemia Mkuu.”
Dk Nchimbi alisema kutokana na hilo, amewafukuza
kazi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Peter Elias ambaye alikuwa Mkuu wa
Upelelezi Mkoa wa Mbeya, Mrakibu wa Polisi, Jacob Kiango aliyekuwa
Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi mkoani humo na Mrakibu Msaidizi wa Polisi,
Charles Kinyongo aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoani
humo.
“Nimemwagiza kiongozi wa polisi awafungulie
mashtaka ya kijeshi askari hawa kwani ajira zao zimesitishwa kuanzia
jana (juzi Jumamosi),” alisema Dk Nchimbi.
Alisema ofisa mwingine aliyefukuzwa kazi kuanzia
jana ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Peter Matagi aliyekuwa Mkuu wa
Upelelezi wa Mkoa wa Kagera kwa kuwapiga na kuwabambikizia kesi zisizo
na dhamana wananchi.
“Mwaka jana kulikuwa na mgogoro wa ardhi katika
Kijiji cha Nyakasimbi huko Kagera kati ya wanakijiji na mmiliki mmoja wa
shamba, wananchi waliona kuwa mmiliki wa shamba hilo ana eneo kubwa
hivyo walikubaliana katika mkutano wa kijiji kuingia kwenye shamba hilo
kwa nguvu,” alisema Dk Nchimbi na kuongeza:
“Waliingia na kuanza kuswaga ng’ombe kuelekea kwa
Mkuu wa Wilaya, walikamatwa watu 12 lakini wawili walifanikiwa kutoroka
na walisafiri hadi Dodoma kumwona mbunge wao, ambaye aliomba kuonana na
mimi.”
Dk Nchimbi alisema licha ya kukubali kuonana nao,
ilishindikana baada ya watu hao kukamatwa wakidaiwa kuwa ni majambazi
ambao walikuwa wakitafutwa huko Karagwe.
“Nilimpigia simu Kamanda wa Polisi Kagera nikitaka kuonana na hao majambazi katika Hoteli ya Dodoma na waliletwa na niliwasikiliza na kugundua kuna tatizo la wao kubambikiziwa kesi ya ujambazi wa kutumia silaha ambayo huwa haina dhamana,” alisema.

Alisema aliunda timu ambayo aliiongoza akiwa na
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Aggrey Mwanri na
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole
Medeye na kusimamia uchunguzi na Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali
iligundua hakuna mashtaka kama hayo na ndiyo maana Matagi anafukuzwa
kazi na kushtakiwa kijeshi.
No comments:
Post a Comment