Monday, March 11, 2013

Mwanamke auawa akila chakula cha usiku



 


Kwa ufupi
Ngidindi alisema baada ya watu hao kumvamia walimshambulia kwa kumkata kwa mapanga sehemu za kichwa chake hadi ubongo kumwagika chini


Sengerema. Watu wawili wasiojulikana majina yao na walikotoka wamemuua  Juliana Masele (55) mkazi wa Kitongoji cha Senta A, katika Kijiji cha Bupandwa, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Tukio hilo lilitokea juzi , siku moja baada ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema sherehe hizo zilifanyika katika kata jirani ya Bulyaheke.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa uchunguzi wa kubaini waliohusika na mauaji hayo unafanyika.
Mtoto wa marehemu aliyejitambul;isha kwa jina la Japhet  Masele (36) alisema tukio hilo lilitokea wakati mama yake (Marehemu) akila chakula cha usiku na watoto wake watano ambapo watu wasiofahamika walivamia nyumbani hapo na kufanya mashambulizi hayo kwa kutumia mapanga.
Naye Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho,Vicent Ngidindi  alisema tukio hilo lilitokea baada ya watu wasiojulikana kumvamia nyumbani kwake saa 2:30 usiku wakati akila chakula cha usiku na watoto wake.
Ngidindi alisema baada ya watu hao kumvamia walimshambulia kwa kumkata kwa mapanga sehemu za kichwa chake hadi ubongo kumwagika chini.
Alisema watu hao pia walimkata mkono marehemu na kuudondosha chini na kwamba jeraha hilo lilisababisha damu nyingi kuvuja na kusababisha kiofo.
Alisema watu hao  walikuwa wamevalia makoti marefu na kufunika nyuso zao mithili ya maninja.
Alisema baada ya kumjeruhi mama yao waliondoka pasipo kuchukua kitu chochote wala kumdhuru mtu mwingine na kwamba hakuna taarifa zozote walizoziacha

No comments:

Post a Comment