Monday, March 11, 2013

Mshukiwa wa ubakaji ajinyonga India



 
Maandamano yalifanyuika baada ya ubakaji huo mjini Delhi kulaani kitndo hicho cha unyama

Mshukiwa katika kesi ya ubakaji wa msichana mmoja wa chuo kikuu ambaye baadaye alifariki nchini India, amepatikana amefariki gerezani. Haya yamethibitishwa na wakili wake.
Polisi wanasema kuwa Ram Singh, alijinyonga akiwa ndani ya gereza la Tihar mjini Delhi's Tihar, lakini mawakili wa utetezi wanadai kuwa huenda alinyongwa.
Ram Singh, aliyekua na umri wa miaka 33, alikuwa mmoja wa washukiwa katika kesi ya ubakaji wanaozuiliwa na polisi kwa madai ya mauaji ya msichana waliyembaka.
Wote walikanusha madai hayo.
Shambulizi dhidi ya mwanafunzi huo, lililofanyika Disemba mwaka jana, lilizua mjadala mkali nchini India kuhusu wanawake wanavyodhulumiwa.
Jela la Tahir ambako washukiwa wa ubakaji wanazuiliwa 

Kesi ya mshukiwa wa sita inaendeshwa katika mahakama ya watoto.
Mwandishi wa BBC Sanjoy Majumder,mjini Delhi,anasema kuwa kifo cha bwana Singh kinakuja kama aibu kubwa kwa maafisa ambao wanakabiliwa na shinikizo kubwa kuhusu kesi hiyo.
Msemaji wa jela hiyo Sunil Gupta, aliambia BBC kuwa Ram Singh alijinyonga kwa banketi usiku wa kuamkia leo.

No comments:

Post a Comment