Monday, March 11, 2013

Kenyatta: Demokrasia imedhihirika Kenya



 
Uhuru Kenyatta ni rais wa nne wa Kenya baada ya kutangazwa mshindi Jumamosi

Rais mpya mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametaja ushindi wake kwenye uchaguzi wa Kenya kama ushindi kwa demokrasia na amani.
Baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi uliofanywa Jumatatu, kwa kupata asilimia hamsini nukta sufuri saba, Kenyatta alisema wapiga kura walizingatia sheria na kuahidi kushirikiana na wapinzani wake.
Hata hivyo mpinzani wake mkuu, Raila Odinga, aliahidi kupinga ushindi wa Kenyatta mahakamani.
Aidha bwana Kenyatta , anakabiliwa na kesi ya uhalifi dhidi ya binadamu katika mahakama ya ICC, akidaiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Kenyatta anatuhumiwa kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya watu elfu moja waliuawa na wengine zaidi ya laki sita kuachwa bila makao.
Siku ya Jumamosi, tume ya uchaguzi ilimtangaza Kenyatta kama mshindi wa uchaguzi huo, baada ya kushinda zaidi ya asilimia hamsini kwa njia wazi na huru.
Tume hiyo ilisema kuwa wapiga kura walijitokeza kwa wingi sana asilimia themanini na sita idadi kubwa zaidi ya wapiga kura kuwahi kushuhudiwa.
Ulikuwa uchaguzi wenye ushindani mkali kuwahi kushudiwa vile vile.
Baada ya matokeo kutangazwa,Kenyatta aliambia wafuasi wake kuwa atawahudmia wakenya wote, bila ya mapendeleo.
Baada ya ushindi wake, Uhuru aliwaambia wakenya kuwa kinachosherehekewa ni, ushindi wa demokrasia, amani na umoja.
Aliongoza kuwa wapiga kura walionyesha kukomaa kisiasa kwa kiwango ambacho hakikutarajiwa na kuwataka walioshindwa kushirikiana nao.
Hata hivyo kwa upande wake, Odinga, alisema tume ya uchaguzi iliwakosea wakenya.
Ametangaza kuwa atapinga matokeo hayo katika mahakama ya juu zaidi.

No comments:

Post a Comment