Kundi la watu wapataoo 30
waliokuwa wamejihami kwa bunduki wametumia baruti kushambuliwa jengo
moja lenye ulinzi mkali, Kaskazini mwa Nigeria, na kumteka nyara
mhandisi mmoja raia wa Ufaransa.
Idara ya polisi nchini Nigeria imethibitisha
tukio hilo na kusema kuwa watu wawili waliuawa katika shambulio hilo
lililotokea katika jimbo la Katsina.Mkuu wa polisi katika eneo hilo Abdullahi Magaji, amesema kundi hilo kisha likavamia kituo kimoja cha polisi, ili kuzuia maafisa wa polisi kuwafuata
Jimbo la Katsina limekuwa tulivu na halijaathirika na machafuko yanayoendelea kushuhudiwa Kaskazini mwa Nigeria yanayosababishwa na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram.
No comments:
Post a Comment