Monday, May 5, 2014

Kiongozi wa maandamano Nigeria mbaroni



 
Shule hii ndio waliokuwepo wasichana hao waliotekwa
Mwanaharakati mwanamke aliyekuwa akiongoza maandamano nchini Nigeria kushinikiza serikali ya nchi hiyo kuwaokoa wasichana 200 waliotekwa hivi karibuni ametiwa mbaroni na polisi kwa amri ya mke wa Rais wa nchi hiyo.
Naomi Mutah Nyadar alikuwa miongoni wanawake waliohudhuria mkutano ulioitishwa na ma mke wa rais Patience Jonathan na baadae mwanaharakati huyo alipelekwa kituo cha polisi habari zinasema.

Inasemekana Mke wa Rais Jonathan anahisi mama za wasichana waliotekwa walimtuma mwanaharakati huyo ili aweze kuwawakilisha.
Mke wa Rais wa Nigeria Patience Jonathan
Mchambuzi wa masuala ya Nigeria anasema Mke wa Rais Jonathan ni Mwanasiasa mwenye nguvu nchini Nigeria.
Mama Mutah mwakilishi wa jamii ya Chibok eneo ambalo wasichana hao walipotekwa wakiwa shuleni zaidi wiki mbili zilizopita, wiki iliyopita aliandaa maandamano katika mji mkuu wa Abuja.
Waandamanaji wengi wakiwa ni Wanaigeria wanaona serikali ya nchi hiyo haijafanya vya kutosha kuwatafuta wasichana hao waliotekwa wanaodhaniwa kuwa ni kundi la kiislam la Boko Haram.
Hadi sasa Boko haram hawajasema lolote kuhusu tuhuma hizo.
Wasichana wanne walio mbele ambao ni miongoni mwa waliotekwa na kufanikiwa kutoroka

No comments:

Post a Comment