Watu kadhaa wameripotiwa kufariki baada ya kutokea mkanyagano katika tamasha la kumkumbuka mwanamuziki maarufu wa Congo King Kester Emeneya.
Baadhi ya vyombo vya habari vinasema kuwa zaidi
ya watu 20 wamefariki ingawa maafisa wakuu bado hawajatoa takwimu rasmi
za watu. Maafisa wanasema kuwa mwanamuziki huyo alifariki mjini Paris mapema mwaka huu akiwa na umri wa miaka 57.
Idadi kubwa ya watu ilikusanyika nyumbani kwake mjini Kikwit katika Jamhuri ya kidemokrasia kwa tamasha hilo la kumkumbuka.
Maelfu walihudhuria mazishi ya marehemu nyumbani kwake karibu na mji wa Kinshasa mwezi Machi baada ya kifo chake mwezi Februari kutokana na maradhi ya Moyo.
Shirika la habari la AFP limesema kuwa Emeneya alikuwa mwanamziki mbunifu aliyeanzisha utumizi wa zana za kielektroniki katika muziki nchini Congo.
Tamasha hilo lililotarajiwa kuendelea hadi Jumapili limefutiliwa mbali.
No comments:
Post a Comment