Wafanyakazi raia wa Kenya wa
mashirika ya misaada ya kibinadamu ambao walikuwa wametekwa na wapinaji
wa kiislamu wa Al shabaab mwaka 2011 wameokolewa na majeshi ya Kenya.
Daniel Njuguna ambaye alikuwa akifanya kazi
katika shirika la Madaktari wasio na mipaka Medecins Sans Frontieres MSF
na James Kiarie wa Shirika la Care International, walichunguzwa afya
zao na walitarajiwa kusafirishwa kwenda Nairobi.Awali walikuwa chini ya uangalizi wa majeshi ya Kenya ambalo lipo kwenye kikosi cha Umoja wa Afrika kilichopo nchini Somalia AMISOM.
Kenya ilituma majeshi yake kwenda nchini Somalia mwaka 2011 kujiunga na AMISOM kufuatia matukio ya utekaji nyara yaliyokuwa yakiendeshwa na wapiganaji wa Al shabaab katika mipaka ya nchi hiyo na Somalia.
Majeshi ya AMISOM yakishirikiana majeshi yale ya serikali ya Somalia yamekuwa yakiendesha mapambano dhidi ya wapiganaji wa Al Shabaab ambao wanafadhiliwa na kundi la kigaidi la al Qaeda linaloshikilia maeneo ya kusini na katikati mwa Somalia.
No comments:
Post a Comment