Kivumbi cha michuano ya Kombe la
UEFA, kusaka klabu bingwa Ulaya, kinaendelea Jumanne wakati miamba wa
England, Chelsea watakapopepetana na miamba wa Ufaransa Paris Saint
Germain, PSG katika mchezo wa marudiano hatua ya robo fainali, ambapo
Chelsea watakuwa wenyeji.
Chelsea inatarajia kumtumia mshambuliaji wao
Samuel Eto'o mwenye umri wa miaka 33 ambaye katika mchezo wa awali
ulipigwa mjini Paris, hakucheza kutokana na maumivu ya nyama za paja,
lakini Jumatatu alifanya mMshambuliaji wa pembeni Andre Schurrle, ambaye alitoka nje kutokana na maumivu katika mchezo dhidi ya Stoke Jumamosi huenda akawa imepona na kucheza mchezo wa leo Jumanne.
Chelsea, The Blues wanatarajia kubadilisha matokeo baada ya mchezo wa kwanza kupokea kipigo cha magoli 3-1.
Mchezaji kiungo John Mikel Obi alikosa mchezo dhidi ya Stoke kutokana na kuumia, lakini anaweza kucheza nafasi ya Ramires anayetumikia adhabu ya kadi au kuchukua nafasi ya Nemanja Matic.
Raia huyo wa Sweden, ambaye ametikisa nyavu mara 40 katika ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1 msimu huunafasi yake itazibwa na Edinson Cavani.
Mshambuliaji huyo wa Uruguay, ambaye amejiunga na PSG kwa kitita cha pauni milioni £55, msimu wa kiangazi, ni mchezaji tegemeo katika timu ya PSG ya kocha Laurent Blanc anayetumia mfumo wa uchezaji wa 4-2-3-1.
"Cavani' si tu mshambuliaji anayebaki kupokea mipira katika eneo la hatari, bali pia huzuia, hutafuta mipira na huwatisha wapinzani, hilo ni jambo kubwa kwetu," anasema Blanc.
Michezo mingine ya UEFA Jumanne inazikutanisha timu za Borrusia Dortmund ya Ujerumani na Real Madrid ya Hispania. Katika mechi yao ya awali, Borrusia ilichezea kipigo cha magoli 3-0. Mchezo huo ulifanyika mjini Madrid.
Jumatano Manchester United itakuwa inakabiliana na mabingwa watetezi wa kombe la UEFA Bayern Munich ya Ujerumani katika mchezo wa marudiano katika uwanja wa Allianz Arena.
Mchezo wa awali katika uwanja wa Old Trafford, timu hizo zilifungana goli 1-1.
Mchezo mwingine utakuwa kati ya Atletico Madrid na Barcelona. Timu hizo nazo zilitoka sare ya 1-1.
No comments:
Post a Comment