Mtu mmoja ameuawa katika makabiliano makali nje ya kanisa la kikopti kufuatia mazishi ya wakristo wanne wa kanisa hilo waliouawa katika ghasia za kidini siku ya Alhamisi.
Waombolezaji waliokuwa wanatoka katika kanisa hilo walikabiliana na wenyeji wa eneo hilo nje ya kanisa.
Wizara ya afya ilisema kuwa mtu mmoja aliuawa katika ghasia hizo.Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi kujaribi kuwatawanya waandamanaji. Zaidi ya watu 80 walijeruhiwa kwa mujibu wa shirika la kitaifa la habari.
Waombolezaji awali walikuwa wakiimba nyimbo za kupinga serikali ya rais Mohammed Morsi.
Walioshuhudia vurugu hizo waliambia wanahabri kuwa ghasia zilianza baada ya umati wa watu kuvamia kikundi cha waombolezaji walipokuwa wanaondoka kanisani kwa kuwarushia mawe na mabomu ya petroli. Wakati huo pilisi walikuwa wachache sana katika eneo hilo.
Wakristo nao walijibu mashambulizi dhidi yao kwa kuwarushia mawe watu hao hadi polisi walipowasili katika eneo hilo na kujaribu kusitisha vurugu kwa kuwarushia watu gesi ya kutoa machozi
Duru zilisema kuwa barabara zilizoko karibu na eneo hilo zilikuwa na ghasia kati ya wakristo na watu wasiojulikana
Aidha moto uilianzishwa katika jengo lililokuwa karibu na kanisa hilo lakini moto huo ukazimwa kwa wakati.
Pia inaarifiwa kuwa Rais Morsi alilaani ghasia hizo kupitia kwa njia ya simu kwa papa Tawadros wa pili ambaye ndiye kiongozi kwa kanisa la kikopti.
''Shambulizi lolote dhidi ya kanisa hilo ni kama shambulizi dhidi yangu,'' alisema Papa Towadros ambaye pia aliwataka watu kuwa watulivu.
No comments:
Post a Comment