
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela
Aliyefariki dunia, amefahamika kwa jina la Swaleh Daudi (14),
ambaye ni mwanafuzi wa darasa la tatu katika shule hiyo na mkazi wa
Maramba Mawili.
Waliojeruhiwa ni Victoria Robert (11), ambaye ni mwanafunzi wa
darasa la tano; Sabrina Zubeir Hussein (9) wa darasa la tatu, ambao wote
ni wakazi wa Maramba Mawili na Jesca Gabriel (13) wa darasa la tatu,
ambaye ni mkazi wa Mbezi Kwa Msuguri.
Mwalimu aliyejeruhiwa, amefahamika kwa jina la Rogath Munisi (37),
ambaye yeye na wanafunzi hao walipata mshituko na kupoteza fahamu.
Wote walikimbizwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, kwa matibabu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha
kifo cha mwanafunzi huyo pamoja na wenzake na mwalimu huyo kujeruhiwa.
Alisema wanafunzi na mwalimu huyo waliangukiwa na ukuta huo
walipokuwa katika harakati za kujiokoa baada ya mvua kubwa iliyoambatana
na upepo kunyesha katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam
jana kuezua paa za vyumba vitano vya madarasa ya shule hiyo.
Hata hivyo, alisema kati ya vyumba hivyo, ikiwamo ofisi ya mwalimu mkuu, kimoja kiliharibiwa na mvua hiyo sehemu ndogo.
“Katika kukimbia, ukuta uliangukia watoto wanne na wote walipoteza
fahamu. Ningependa kutoa pole nyingi sana kwa msiba ulioipata familia
iliyofiwa na mwanafunzi huyo. Naomba wawe wastahamilivu katika kipindi
hiki cha msiba. Pia walioko hospitali nawaombea wapone ili waweze
kuungana na familia zao,” alisema Kamanda Kenyela.
Kutokana na tukio hilo, Mku wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck
Sadiki, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana,
walitembelea eneo hilo.
Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati ya Shule hiyo, Aloyce Lukwaro, shule hiyo ina watoto 2,800 na vyumba 13 vya madarasa.
“Tunaelekea kufanya mtihani wa darasa la nne na saba. Hali ni mbaya
sana. Hatujui shule watasomaje na watasimamiwaje,” alisema Lukwaro.
No comments:
Post a Comment