>>BARCA KUPINDUA KICHAPO 2-0 CHA AC MILAN??
>>TAYARI ROBO FAINALI: REAL, DORTMUND, JUVE & PSG!
>>NANI KUUNGANA NAO??
JUMANNE na JUMATANO Usiku zipo Mechi 4
za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, lakini kwa
Jumanne, macho, masikio na kila kitu kitakuwa huko Nou Camp kushuhudia
kama ile inayodaiwa Timu Bora Duniani, FC Barcelona, itaweza kupindua
kipigo cha Bao 2-0 na kuibwaga nje AC Milan.
+++++++++++++++++++++++++++
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
RATIBA:
-Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumanne 12 Machi 2013
Barcelona v AC Milan [0-2]
Schalke v Galatasaray [1-1]
Jumatano 13 Machi 2013
Bayern Munich v Arsenal [3-1]
Malaga v FC Porto [0-1]
+++++++++++++++++++++++++++
AC
Milan, inayoongozwa na Kocha Massimiliano Allegri, inatumbukia Nou Camp
kuivaa Barcelona baada ya kuifunga Bao 2-0 katika Mechi yao ya kwanza
kwa Bao za Kevin-Prince Boateng na Sulley Muntari Uwanjani San Siro.
Barca,
baada ya kufungwa na AC Milan, ilipata pigo kubwa ilipofungwa mara mbili
mfululizo ndani ya Wiki moja na Mahasimu wao wakubwa Real Madrid,
kwanza kwa Bao 3-1 na kubwagwa nje ya Copa del Rey na kisha 2-1 kwenye
La Liga, lakini juzi Jumamosi iliifunga Deportivo La Coruna Bao 2-0
kwenye La Liga.
Nao AC Milan, majuzi Ijumaa,
walliwachapa Genoa Bao 2-0 kwenye Mechi ya Serie A lakini walipata pigo
kubwa pale Straika wao wa kutegemewa, Giampaolo Pazzini, alipovunjika
mfupa wa mguu na pia hawawezi kumchezesha Straika wao mwingine Mario
Balotelli ambae ameshacheza Mashindano haya Msimu huu akiwa na
Manchester City.
+++++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
-KLABU hizi zimekutana mara 16, Barca wakishinda mara 6 na AC Milan mara 5 huku Barca wakipiga Bao 22 na AC Milan 21.
-NOU CAMP: Barca Wameshinda Mechi 3 Sare 3 na AC Milan Wameshinda 1
-MSIMU uliopita walikutana Robo Fainali
ya UCL wakatoka 0-0 huko San Siro na Barca kushinda 3-1 Nou Camp kwa Bao
2 za Penati za Lionel Messi na moja la Iniesta huku Bao la AC Milan
kufungwa na Antonio Nocerino.
-MSIMU WA 2011/12 walikuwa Kundi moja na Mechi ya kwanza Nou Camp ilikuwa 2-2 na huko San Siro Barca walishinda 3-2
+++++++++++++++++++++++++++
Kocha wa
muda wa Barcelona, Jordi Roura, ambae anashikilia wadhifa huo kwa vile
Kocha Mkuu Tito Vilanova yuko kwenye matibabu ya ugonjwa wa Kansa,
ametoa onyo kuwa Wachezaji wake wako tayari kwa changamoto hii ya AC
Milan
No comments:
Post a Comment