Wednesday, March 6, 2013

SENTENSI TATU ZA JAMES MBATIA BAADA YA KUITWA KTK TUME YA KUCHUNGUZA MATOKEO YA FORM IV







.
.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na mbunge wa kuteuliwa James Mbatia, amesema hayuko tayari kuwa mjumbe wa tume ya kuchunguza chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwenye mitihani ya kidato cha nne 2012 kutokana na kutoona umuhumu wa kuchunguzwa kwa hayo matokeo.
Amesema anashangazwa na kitendo cha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuunda tume ya kuchunguza matokeo hayo wakati ripoti ya uchunguzi wa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2011 ilishawasilishwa ofisini kwa Waziri mkuu lakini mpaka leo haijafanyiwa kazi.
Namkariri akisema “Kwenye tume aliyounda Mh Waziri mkuu, kwa heshima zote na unyenyekevu mkubwa tu na heshima waliyonipatia, mimi niko kwenye benchi la Bunge na hoja yangu bado iko bungeni, mimi nina mgogoro na Serikali kwamba hakuna mitaala alafu nikachunguze Mitaala ambayo mimi siiamini na sijui ipo, nikachunguze kitu gani? nasema haipo…. sasa unanipeleka kwenye tume nikale matapishi yangu mwenyewe? mimi ni raia wa Tanzania nina haki ya kutetea nchi yangu, nilikula kiapo cha kuwa mtiifu kwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania sio kwa Serikali

No comments:

Post a Comment