Saturday, March 16, 2013

Rais Kikwete aonja adha ya kukatika umeme Morogoro





Morogoro. Adha ya kukatika mara kwa mara kwa umeme mjini Morogoro, imemkumba pia Rais
Jakaya Kikwete mara baada ya umeme huo kukatika muda mfupi alipoingia katika Ukumbi wa Magadu unaomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kambi ya Mzinga kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kigurunyembe, Jimbo la Morogoro.
Hali hiyo, ilitokea  saa 2:20 usiku wakati Askofu wa kanisa hilo, Mhashamu Telesphor Mkude, alipokuwa akiombea mkutano huo na katikati ya maombi yake umeme ulikatika ghafla na kufanya ndani ya ukumbi huo kuwa giza totoro.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya umeme huo kukatika mashine ya dharula ya kuzalisha umeme (jenereta)  iliwashwa na umeme kurejea na kumwezesha askofu Mkude kuhitimisha.

No comments:

Post a Comment