Sunday, March 3, 2013

Miji miwili yakombolewa Congo

Jeshi la Jamhuri ya Demokrasi ya Congo linasema kuwa limeikomboa miji miwili ya mashariki mwa nchi ambayo ilikuwa imedhibitiwa na wapiganaji wa M23 kwa miezi kadha.
Polisi wa Congo mjini Rutshuru
Msemaji wa jeshi alieleza kuwa wanajeshi wa serikali wameingia katika miji ya Rutshuru na Kiwanja baada ya M23 kuondoka.
Juma hili M23 waligawanyika mapande mawili ambayo yalianza kupigana.
Maelfu ya watu wamekimbilia nchi ya jirani, yaani Uganda, ili kuepuka mapigano hayo.
Mapambano yalianza punde baada ya viongozi wa Afrika kutia saini mkataba wa kumaliza vita vya miongo miwili mashariki mwa Congo.

No comments:

Post a Comment