
Michael Owen astaafu
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya England,Michael Owen ametangaza kutundika daruga ama kupumzika kucheza soka la ushindani mwishoni mwa msimu huu. Hii imekuwa ni ghafla,lakini wachambuzi wengi wa soka na mashabiki wa mchezo huo ulimwenguni walitarajia taarifa hii.
MICHAEL Alianzia wapi?
Alianza kuwika akiwa na kikosi cha Liverpool na dunia ilimtambua zaidi kwenye miaka ya 1998 akiwa na umri wa miaka 18 wakati alipoitwa kwenye kikosi cha England kilichoshiriki kombe la Dunia mwaka huo na bao lake la pekee dhidi ya Argentina kwenye michuano hiyo lilimpa umaarufu zaidi kabla ya kufunga mabao matatu peke yake maarufu kama hat trick katika mechi ambayo England iliwafunga Ujerumani kwa mabao 5-1 mwezi Septemba mwaka 2001.Hadi hivi sasa Owen amekwisha funga jumla ya magoli 220 kwenye klabu alizochezea,Huku akitwaa Mataji ya Ligi kuu soka nchini England,Kombe la FA,Kombe la Ligi mara tatu na kombe la Uefa.
Mwaka 2001,Owen alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya,akiwa ni Muingereza wa kwanza kutwaa tuzo hiyo baada ya Kevin Keegan aliyetwaa kwenye miaka ya 1976.
Mwaka 2005,Owen alipata majeraha makubwa ya kifundo cha mguu wake akiwa anaichezea timu yake ya taifa,Toka hapo amekuwa ni mwenye kusumbuliwa na majereha ya mara kwa mara.

Michael Owen astaafu
Michael Owen,amezishukuru klabu zake zote alizowahi kuchezea pamoja na mashabiki wake toka akiwa Liverpool mpaka sasa Stoke ambapo amesema kwa sasa hana tena miaka 18 na hana budi kuachana na soka la ushindani,aliandika katika mtandao wake.
Pamoja na yote,Owen atandelea kukumbukwa na waingereza wote kutokana na kipaji chake pamoja na bao lake pekee na la muhimu katika michuano ya kombe la dunia dhidi ya Argentina.
No comments:
Post a Comment