Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka raundi ya pili ya uchaguzi.
Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo
kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada ya
wakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu na
kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.Hata hivyo tume ya uchaguzi ilitarajiwa kutangaza matokeo rasmi baadaye leo mwendo wa saa tano lakini kama inavyoonekana huenda tangazo hilo likachelewa
Popote ulipo kama mkenya au mwana Afrika Mashariki tupe maoni yako kuhusu yanayojiri pale ulipo
15:41 Rais mteule Uhuru Kenyatta anajiandaa kuwahutubia wafuasi wake katika chuo kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki viungani mwa mji wa Nairobi punde tu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu
15:11 Rais mteule Uhuru Kenyatta akabidhiwa cheti cha kushinda uchaguzi mkuu na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Isaack Hassan
14:37 Isaack asema kulingana na katiba ya nchi mshindi lazima apate nusu ya kura zilizopigwa na kwa hivyo Uhuru Kenyatta ambaye alipata kura milioni sita nukta moja ikiwa ni nusu ya kura milioni mbili zilizopigwa, na bila shaka anakuwa rais wa nne wa jamuhuri ya Kenya
14:32 Isaack amesema kuwa kama tume waliamua kutumia mbinu ya zamani kuhesabu kura kwa sababu ya matatizo waliyoyapata kutokana na mitambo yake ya kupeperusha matokeo kugoma. Lakini matokeo yalithibitishwa kwa mujibu wa fomu za hesabu ya kura
14:27 Isaac amepongeza vyombo vya habari vya Kenya kwa walivyopeperusha matangazo yote kuhusu uchaguzi wa Kenya.
14:25 Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Isaack Hassan awahutubia wakenya wakati akijiandaa kutangaza mshindi, wa uchaguzi
14:18 Afisaa mkuu mtendaji wa tume ya uchaguzi ya Kenya James Oswago amesema kuwa uchaguzi uliofanyika Kenya ulikuwa mgumu zaidi kuwahi kufanyika na ulikuwa na changamoto kubwa kuwahi kushuhidiwa Afrika
14:20 Tume ya uchaguzi yajiandaa kutangaza matyokeo ya mshindi wa uchaguzi wa urais
12:39 Lori lililokuwa limewabeba wafuasi wa Uhuru Kenyatta kutoka ngome yake ye Nyeri hususan eneo la Tetu, limeanguka, watu kumi wamejeruhiwa vibaya, mmoja amefariki na wengine zaidi ya 21 wanaendelea kupata matibabu
11:32 Tume ya uchaguzi Kenya inatarajiwa wakati wowote kuanzia sasa kutangaza rasmi matokeo ya kura za urais
11:31 Mwandishi wa BBC Karen Allen kupitia twitter anasema moja ya kauli aliyoisikia leo ambayo imemfurahisha sana ni kumsikia mtu akisema kuwa wakenya ndio wameshinda uchaguzi kwa sababu wana taasisi mpya
09:51 Mjini Eldoret moja ya vitovu vya ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007, leo ni uwanja wa sherehe za ushindi wa Uhuru Kenyatta. Bendera na kila aina ya mabango zinazobebwa na wafuasi wa Kenyatta ni ishara ya furaha yao. Eldoret pia ni ngome ya mgombea mwenza wa Kenyatta, William Ruto
09:23 Mwandishi wa BBC mjini Kisumu ambayo ndio ngome kuu ya Raila Odinga, Ann Mawathe anasema kuwa wafuasi wa Odinga wamenuna kwa kuwa mgombea wao ameshindwa kwenye uchaguzi lakini wanaendelea na shughuli zao kama kawaida
08:45 Mjini Nyeri moja ya ngome za Uhuru Kenyatta ni vifijo na nderemeo tupu barabarani kusherehekea ushindi wake
08:12 Mjini Nakuru mamia ya watu waliamka asubuhi na mapema kusherehekea barabarani kafuatia taarifa za mgombea wao wa urais Uhuru Kenyatta. Wameonekana wakibeba mabango na matawi kama ishara ya furaha yao
08:06 Josiah Mayaka Wa Kisii Kenya anasema kuwa watu wengi Kisii wamesononeka sana ila kwa sababu limetendeka wamekubali matokeo shingo upande.
07:47 Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wameimba wimbo wa taifa wakiwa kando ya majengo ya bunge kusherehekea ushindi wa mgombea wao
07:35 Hanif Mohhamed wa Mombasa-Kenya naona mustakabali wa Kenya ni giza tupu, saa hii anasema anatafakari njia mubadala ya kukumbana na changa moto zitakazo wapata kama wakenya baada ya athari kuanza kuchimbuka.
07:26 Vifijo na nderemeo pamoja na milio ya honi katika barabara ya Kijabe mjini Nairobi kufuatia ushindi wa Uhuru Kenyatta
07:08Alex Mulwa anasema kuwa wakenya wamechagua viongozi ambao wataleta maendeleo na kuleta mabadiliko katika nchi yao. Alex ,kwa niaba ya wakenya anaomba ICC isitishe na kusimamisha kesi dhidi ya Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto ili kuwapa nafasi kuongoza bila wasiwasi
06:55 Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wameanza kujitokeza katika baadhi ya sehemu za mji mkuu Nairobi kusherehekea ushindi wake
06:46 Uhuru Kenyatta ana kura 6,173,433 wakati Raila Odinga 5,340,54. Hii inampa Uhuru ushindi wa asilimia hamsini nukta tatu ambao unahitajika chini ya katiba mpya kwa mtu kushinda uchaguzi wa rais.
06:40 Tume ya uchaguzi baadaye leo itatangaza mshindi wa uchaguzi ingawa hesabu ya kura inaonyesha Uhuru Kenyatta anaongoza kinyang'anyiro.
No comments:
Post a Comment