Thursday, March 7, 2013

Marehemu Chavez apewa heshima za mwisho



 
Mwili wa Chavez ukipitishwa katika barabara za mji mkuu Caracas

Mwili wa mareheu rais Hugo Chavez wa Venezuela, umelazwa katika kituo cha mafunzo ya jeshi katika mji mkuu Caracas
Mapema leo mwili wa marehemu Chavez ulipitishwa kwenye umati mkubwa wa wafuasi wake katika mitaa ya mji mkuu Caracas.
Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia .
Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa heshma zao .
Makamu wa rais Nicolas Maduro anaongoza shughuli hiyo.
Mwili wa rais Chavez umepelekwa katika chuo cha kitaifa cha mafunzo ya kijeshi ambapo utazikwa kesho Ijumaa.
Bwana Chavez alifariki akiwa umri wa miaka 58 baada ya kuugua Saratani kwa zaidi ya miaka miwili.
Maelfu ya watu awali walikwenda barabarani mjini Caracas kutoa heshima zao za mwisho kwa Chavez wakifuatana na gari lililokuwa limebeba jeneza lake kuelekea katika chuo cha mafuzno ya jeshi.
Mazishi ya kitaifa ya Chavez yatafanyika Ijumaa.
Mkuu wa ulinzi wa Rais alinukuliwa akisema kuwa alikuwa na bwana Chavez alipofariki.
Generali Jose Ornella, alisema kuwa Chavez alifariki kutokana na mshtuko wa moyo na katika siku zake za mwisho kabla ya kifo cha ealisema angependa kuendelea kuishi.
Jeneza lake lililokuwa limefunikwa bendera ya nchi hiyo uliwekwa katika ukumbi ambao ni kumbukumbu ya waliopigania uhuru wa watu wa Amerika ya Kusini
Maelfu ya watu walipanga foleni kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Chavez, wakiwemo maafisa wa serikali na viongozi wa Amerika ya Kusini,kama Rais wa Bolivia Evo Morales na Rais wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner.

No comments:

Post a Comment