Thursday, March 28, 2013

Makundi yawadhulumu wakimbizi Somalia


 
Wanwake wengi wamelalamika sana wakisema wanabakwa na watu waliovalia magwanda ya jeshi

Shirika la kutetea haki za kibinadamu, Human Rights Watch, limesema kuwa makundi yaliyojihami nchini Somalia ikiwemo majeshi ya serikali, yamefanya vitendo vya ubakaji, kuwachapa na kuwadhulumu watu walioachwa bila makao au wakimbizi.
Ripoti ya shirika hilo imegusia wale watu waliokimbia vita tangu mwaka 2011 kwa sababu ya njaa, na sasa wanaishi katika kambi mjini Mogadishu.
Katika ripoti hiyo mpya, shirika hilo limesema kuwa wasimamizi wa kambi hizo , wanaojulikana kama walinzi, huiba msaada wa wakimbizi hao na hata kuwadhulumu.
Shirika hilo linasema , kuwa wakimbizi wa ndani, hasa wanawake wameripoti kubakwa na kudhulumiwa na watu waliovalia sare za kijeshi na wengine wanaoaminiwa kuwa wapiganaji wa makundi ya waasi.
Linasema kuwa baadhi ya vitendo vibaya vya dhuluma walivyofanyiwa ni pamoja na dhulma za kingono dhidi ya wanawake na wasichana.
Kadhalika ripoti hiyo imewanukuu wanawake wanaodai kubakwa akiwemo mwanamke mwenye umri wa miaka
23 aitwaye, Quman.

No comments:

Post a Comment