Friday, March 15, 2013

Katiba mpya Zimbabwe? Kura yafanyika leo


 

 

Hapiga kura katika foleni
Zimbabwe inapigia kura ya maoni kielelezo cha katiba hii leo, ikiwa ni mara ya kwanza tangu uchaguzi ufanyike nchini humo uliokumbwa na utata mwaka wa 2008.
Hata hivyo malalamiko yametolewa kuwa huenda nchi hio haijajiandaa vilivyo kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha na wachunguzi wanadai kuwa wamefungiwa nje ya shughuli hiyo.
Mugabe na Tsvangirai
Lakini kwa mara ya kwanza inaonekana kuwa hakuna kizungumkuti kikubwa katika kura hii. Chama chake rais Robert Mugabe ZANU - PF na kile cha upinzani ambacho sasa kiko katika serikali ya muungano MDC, vyote vinaunga mkono kielelezo hicho cha katiba.
Katiba hiyo inapendekeza kuhifadhiwa nafasi ya rais mwenye nguvu nyingi serikalini na hii inampa rais Mugabe uwezo wa kusalia madarakani kwa miaka kumi zaidi.
Hata hivyo kura hii ya maoni haijawachangamsha sana wananchi wa Zimbabwe huku raia wengi wakionekana kulenga zaidi uchagzui mkuu unaopangwa kufayika miezi chache zijazo.
Bendera ya Zimbabwe
Katiba mpya inatazamiwa kunyoosha njia ya kufanyika uchaguzi huo mkuu japo kuna wasiwasi kwa machafuko zaidi kutokea nchini

No comments:

Post a Comment