Uhalifu wapungua mkoani Arusha
Jeshi la polisi mkoani Arusha limetoa mchanganuo wa matukio yaliojiri mwaka 2012 na kusema kuwa ajali za barabani zinaongoza kwa matukio mengi ambayo yamesababisha majeruhi pamoja na vifo kwa watanzania kuliko makosa mengine
Haya yamesemwa na kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alipozungumza na waandishi wa habari nakutanabahisha kuwa matukio yakiuhalifu yalipungua ukilinganisha na mwaka 2011 ambapo mwaka huo ulikuwa na asilimia 16% nakupungua hadi 8.7% kwa mwaka 2012
Aidha kamanda Sabus ameongeza kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa usimamizi wa sheria za usalama barabarani utapewa mkazo zaidi mwaka 2013, na kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani mashuleni pamoja na kukagua leseniza madereva
Vilevile kamanda wa polis ameahidi kutoa zawadi ya pesa taslimu shilingi millioni moja kwa mtu atakae toa taarifa kumpata mtu alie husika na tukio lamlipuko unaosadikiwa kuwa ni bomu la kutengenezwa kienyeji katika chumbaanachoishi katibu wa bakwata mkoa wa Arusha Bw.Abdulkarim Idd Jonjo mwenye miaka 52 nakumsababishia madhara kwenye mwili wake
No comments:
Post a Comment